22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mchezaji Zesco aiuma sikio Yanga  

luizio-1Na ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka kwenye klabu ya Zesco, Juma Luizio, amewauma sikio Yanga kwa kusema kuwa iwapo wanawahitaji wachezaji wao ni vizuri kufanya haraka na kufuata taratibu, kwa kuwa baadhi yao wana mikataba ya zaidi ya mwaka mmoja.

Kwa takribani wiki moja sasa, kumekuwepo na taarifa za Yanga kutaka kulibomoa benchi la ufundi la Zesco kwa kumleta kocha George Lwandamina.

Mbali na hilo, zipo tetesi zinazodai kuwa Yanga wapo kwenye mawindo ya beki Meshack Chaila, Wakenya Jesse Were anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliji na beki David Odhiambo ‘Calabar’, kiungo mchezeshaji Cletus Chama pamoja na Mnigeria Ayo Oluwafami.

Luizio ameliambia MTANZANIA Jumapili kuwa ili Yanga iweze kuwapata wachezaji hao, ni wakati wa kuzungumza nao na kuchukua maamuzi ya haraka, kwani zipo timu  zinazowasaka na iwapo wakichelewa upo uwezekano wa kuwakosa.

Alisema mbali na hilo, wanatakiwa pia kufuata taratibu za kununua wachezaji kwa kuzungumza na uongozi wa Zesco mapema, kwani kati ya wanaotajwa kuhitajika na Yanga wapo mwenye mikataba ya zaidi ya mwaka mmoja.

“Oluwafami na Chaila wao wamebaki na mwaka mmoja na nusu kumaliza mikataba yao, hivyo kama Yanga inawahitaji ni vizuri wakafuata taratibu za kununua wachezaji na si kuzungumza nao, Zesco wakifanikiwa kupata ushahidi juu ya wachezaji wao wenye mikataba kuzungumza na timu nyingine ni lazima wataishtaki Yanga, jambo litakalosababisha kuwakosa wachezaji hao,” alisema.

Alisema kuhusu Odhiambo, Jesse Were na Chama, hawa wapo karibu na kocha Lwandamina, lakini mikataba yao na Zesco inamalizika baada ya ligi, lakini tayari mameneja wao wamefanya mazungumzo na timu kutoka Misri na Afrika Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles