22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Arsenal yaichapa Sunderland nyumbani

giroud_0LONDON, ENGLAND

MICHUANO ya Ligi Kuu nchini England iliendelea jana kwenye viwanja mbalimbali, huku mchezo wa awali uliwakutanisha Sunderland ambao walikuwa nyumbani na kupokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Arsenal.

Arsenal walikuwa wa kwanza kupata bao la kwanza katika dakika ya 19, ambalo liliwekwa wavuni na mshambuliaji wake Sánchez Sánchez, baada ya kazi iliyofanywa na Oxlade-Chamberlain.

Bao hilo lilidumu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza, lakini baada ya kipindi cha pili kuanza, Arsenal walionekana kuridhika na matokeo, wakati huo Sunderland wakionekana kupambana kutafuta bao la kusawazisha, walifanikiwa kusawazisha katika dakika ya 65 kwa mkwaju wa penalti ambao ulipigwa na Jermain Defoe.

Baada ya bao hilo, Arsenal walifanya mabadiliko dakika ya 69, ambapo aliingia Olivier Giroud kuchukua nafasi ya Alex Iwobi. Mabadiliko hayo yalikuwa na faida kubwa kwa Arsenal, ambapo Giroud aliweza kuipa bao la pili katika dakika 71, huku akitumia dakika mbili tangu kuingia.

Dakika tano baadaye Giroud aliweza kuongeza bao la tatu katika dakika ya 76, ambapo alifunga kwa kichwa, hata hivyo, dakika ya 78 Arsenal waliweza kuongeza bao la nne lililofungwa na Sanchez, baada ya kuwatoka mabeki.

Mabao hayo yaliwafanya mashabiki wa Sunderland kuanza kuondoka uwanjani kabla ya mchezo huo kumalizika, huku wakiamini kuwa timu yao haiwezi kupata mabao zaidi ya Arsenal katika mchezo huo.

Hadi sasa Sunderland inashika nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi Kuu nchini England, ikiwa na alama 2 baada ya kucheza michezo 10, wakati huo Arsenal ikiwa kileleni mwa Ligi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles