
LAGOS, Nigeria
KWA nyakati tofauti, Funke Etti, amekuwa akisemwa kwa madai ya kutumia mafuta ya kujichubua ngozi ‘mkorogo’, lakini mwigizaji huyo amekanusha madai hayo.
Funke alisema yeye hupenda kutumia mafuta ya kawaida ambayo hutumika na mwanamke yeyote kwa ajili ya kung’arisha ngozi na hatumii mkorogo.
“Sijichubui na si kweli kwamba niliwahi kutoa ushauri kwa wanawake wenzangu kuwa kutumia mkorogo ni vizuri.
Kama mimi situmii, kwanini niwashauri wengine kufanya hivyo? Mimi mwenyewe sipendelei hicho kitu. Huwa natumia mafuta ya kawaida ya urembo yanayotusaidia wanawake kung’aa. Hicho ndicho ninachoweza kusema,” alisema.