23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

UEFA yawaonya mashabiki Urusi, England

Mashabiki wa uingereza na Urusi wakivutana wakati timu zao zilipokuwa zinacheza juzi.
Mashabiki wa uingereza na Urusi wakivutana wakati timu zao zilipokuwa zinacheza juzi.

PARIS, Ufaransa

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya (UEFA), limewaonya mashabiki wa timu za taifa za England na Urusi ambao walihusika kwenye fujo zilizotokea kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kundi B wa michuano ya Euro ambao ulimalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.

UEFA liliwaeleza mashabiki hao kuwa iwapo wataendeleza fujo zao hizo watashuhudia timu zao zikiondolewa kwenye michuano hiyo.

Hivi karibuni shirikisho hilo lilianza mchakato wa kuichukulia hatua za kinidhamu Urusi kutokana na wao ndio kuanzisha fujo hizo dhidi ya mashabiki wa England mara baada ya mchezo baina yao kumalizika.

“Kamati ya utendaji ya UEFA imezionya bodi za kusimamia nidhamu kwa pande zote mbili kuwa makini na suala hili, kwani iwapo fujo hizi zitaendelea, basi kamati haitasita kuchukua hatua stahiki, ikiwamo kuziondoa kwenye mashindano timu husika,” ilisema UEFA katika tamko lake.

“Tunaziomba FA ya England na shirikisho la soka la Urusi zipingane na tabia wazifanyazo mashabiki wao kwani hazikubaliki katika michezo.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles