27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

Murray arejea kwa kocha wake wa zamani

Andy Murray
Andy Murray

EDINBURGH, SCOTLAND

MCHEZAJI wa tenisi, Andy Murray, hatimaye ameungana tena na kocha wake wa zamani, Ivan Lendl, kabla ya michuano ya Aegon.

Murray mwenye miaka 29, alikuwa bila kocha huyo muda mfupi kabla ya kuanza kwa michuano ya wazi ya Ufaransa mwezi uliopita.

Mskoti huyo ambaye aliwahi kuwa namba moja kwenye mchezo huo akiwa na kocha Ivan Lendl, alishinda michuano ya wazi ya Wimbledon na michuano ya wazi ya Marekani ya Olimpiki katika kipindi cha miaka miwili 2012-2014.

Lendl ni mshindi namba moja duniani na mshindi mara nane wa Grand Slam na aliwahi kuwa mtumishi katika Shirikisho la Tenisi la Marekani.

Tangu kutengana kwao mwaka 2014, Murray alifanikiwa kufika  fainali ya michuano mikubwa mara tatu ikijumuishwa na French Open ambayo Novak Djokovic aliibuka kuwa bingwa.

Murray alitangaza kutengana na kocha wake wa sasa, Amelie Maueresmo, mwezi mmoja uliopita na baadaye alikuwa chini ya kocha Jamie Delgado wakati alipokuwa jijini Paris Ufaransa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,409FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles