22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Efm yatenga Sh milioni 3 kwa mashabiki wake

e fmNA ASIFIWE GEORGE,

KITUO cha Redio Efm kimetenga jumla ya Sh milioni 3 kwa washindi wa mchezo wa Sakasaka 2016 unaofanyika kwa mwaka wa pili baada ya kupata mafanikio mwaka jana.

Mkuu wa Kitengo cha Matukio na Mawasiliano, Neema Mukurasi, alisema shindano hilo huchezeshwa kwa kuficha  kitu katika eneo mojawapo kisha msikilizaji wa redio hiyo hutakiwa kusikiliza maelekezo kisha kwenda kutafuta kitu hicho kilichofichwa ndipo hujishindia zawadi hizo.

Alisema mchezo huo kwa mwaka huu unatarajiwa kuanza Juni 12 kwa wilaya tano, Kinondoni, Ilala, Temeke, Mkuranga na Kisarawe.

“Idadi kubwa ya wasikilizaji wetu wana changamoto nyingi za maisha hivyo sisi Efm tunawawezesha kupitia vitu tofauti tofauti ambavyo vitawasaidia kujikwamua kimaisha,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles