28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Everlyn Felix ashinda Miss Albino Tanzania

Everlyn Felix
Everlyn Felix

NA GEORGE KAYALA,

USIKU wa Juni 10, kwenye Ukumbi wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF) mkoani Dodoma, utakuwa wa ukumbusho mkubwa kwa mrembo Everlyn Felix mkazi wa Arusha kutokana na kutangazwa kuwa Miss Albino Tanzania  2016.

Kutokana na ushindi huo mrembo huyo amepokea zawadi ya Sh 500,000.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Diana Kessy naye kutoka Arusha aliyejinyakulia kitita cha Sh 300,000 huku Zawadi Doto mkazi wa Mwanza akishika nafasi ya tatu na kujizolea Sh 200,000.

Katika fainali hiyo washindi wa kwanza na wa pili waliopatikana utoka mikoa ya Kanda ya Mashariki, Ziwa na Kaskazini walishindanishwa huku mgeni rasmi akiwa Mbunge wa Kilolo mkoani Iringa, Venance Mwamoto, aliyeahidi kuishawishi Serikali kuondoa kodi inayotozwa kwenye mafuta yanayotumiwa na albino.

Mratibu wa shindano hilo, Fredy Kaula, alisema kulikuwa na changamoto kubwa katika uendeshaji wa shindano hilo ikiwemo mwitikio mdogo wa washiriki huku akiamini mwaka unaofuata idadi ya washiriki itaongezeka kwa kuwa pia zawadi zitaongezeka kwa washindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles