28.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

EFM yazindua mziki mnene

Efm-logo-jpg-1024x542NA ASIFIWE GEORGE

KITUO cha Utangazaji cha EFM kimezindua mradi wake wa ‘Mziki Mnene’ utakaokuwa ukifanyika katika bar mbalimbali kuanzia Septemba 5 mwaka huu.

Meneja mkuu wa mawasiliano wa kituo hicho, Denis Ssebo, alisema wamepanua wigo kwa wasikilizaji wa redio hiyo na sasa watawafikia watu wengi kwa kuwa bar 12 zitatembelewa.

Alitaja maeneo watakayofika ni Kibaha, Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe, Kigamboni na mengine mengi ambayo wanaamini wana mashabiki wakutosha.

Alisema baada ya uzinduzi huo, Septemba 28 watahitimisha kwa tamasha kubwa ambalo litakuwa na vionjo mbalimbali.

“Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula kwasababu tutawafikia na kuwamiminia burudani ambayo pia itarushwa ‘live’ kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha EFM,” alisema Ssebo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,324FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles