24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Honeymoon aeleza siri ya tuzo zake za ZIFF

Muongozaji bora wa filamu, HoneymoonJULIET MORI NA LETICIA BWIRE (TUDARCO)

MSHINDI wa tuzo mbili za kimataifa za filamu alizozipata katika Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), Honeymoon Mohammed, amesema filamu bora inatokana na uandishi wa muswada (script), mandhari nzuri pamoja na uwezo wa msanii husika.

Tuzo hizo alizopata kutokana na filamu yake ya ‘Daddy’s Wedding’ ni filamu yenye picha bora na mwongozaji bora wa filamu.

Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) jana, Honeymoon alitolea mfano wa filamu yake hiyo iliyoshinda tuzo mbili kwamba ilitokana na uandishi bora wa muswada, uongozaji na pia mandhari bora ya utalii aliyotumia katika hifadhi ya Saadan.

“Kilichoifanya filamu yangu ishinde ni mandhari niliyotumia katika filamu yangu, nimetumia hifadhi ya Saadan tofauti na wasanii wengine wanavyopenda kutengenezea filamu zao kwenye majumba ya kifahari ambayo hukosa uhalisia wa maisha halisi ya wanachokiigiza,” alisema Honeymoon.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles