28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mr Flavour kama Diamond, apata mtoto

flavour nabaniaWAKATI nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul (Diamond Platinum) akifurahia mtoto wake wa kwanza aliyempa jina la Tiffah, nyota mwenzake wa Nigeria, Flavour Nabania ‘Mr Flavour’ naye amepata mtoto.

Diamond Platinum na mpenzi wake, Zarina Hassani (Zari), wamefanikiwa kupata mtoto wa kike huku Mr Flavour na mpenzi wake, Anna Banner wakipata mtoto wa kiume.

Mtoto wa Mr Flavour amezaliwa Texas nchini Marekani akiwa ni mtoto wake wa pili, wa kwanza akiwa amezaa na mrembo, Sandra Okagbue, mwaka jana huku mpenzi wake, Anna mwenye miaka 20 akiwa ndiye mtoto wake wa kwanza.

Kama ilivyo kwa Diamond akifurahia mtoto wake wa kwanza huku Zari akiwa na mtoto wa nne.

Anna alikuwa akisoma Dubai lakini alikacha masomo baada ya kuahidiwa ndoa na Mr Flavour, lakini msanii huyo aliwahi kutangaza kwamba hana mpango wa ndoa kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles