25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kerr ampa jukumu zito Hanspope Simba

dylanker-haiphongNA SAADA SALIM, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, ameipa jukumu zito kamati ya usajili ya klabu hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti, Zacharia Hanspope, kuhakikisha wanasajili mshambuliaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba ina washambuliaji; Khamis Kiiza, Ibrahim Ajibu, Elias Maguli na Mussa Hassan ‘Mgosi’, lakini agizo hilo la kocha limetokana na ubutu ulioonekana katika timu yake.

Katika mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya Sports Club Villa Uwanja wa Taifa, Simba ilicheza kwa kiwango kikubwa sana lakini umaliziaji uliiangusha timu hiyo na kutoka uwanjani na ushindi mwembamba wa bao 1-0.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kerr alisema anahitaji mshambuliaji mwenye uchu wa kufunga mabao mengi zaidi kabla ya dirisha la usajili kufungwa Agosti 20 mwaka huu.

Kerr alisema pamoja na klabu hiyo imefanya usajili mzuri, lakini anahitaji kuona anapata mshambuliaji mwenye uwezo wa kusumbua mabeki ambao wako vizuri.

“Kulingana na mechi za kirafiki ambazo timu yangu imecheza, imeonyesha kiwango kizuri lakini nimeona tatizo kwenye umaliziaji ambapo nahitaji kupata mshambuliaji mwenye uchu wa kufumania nyavu, kwani bado nahitaji mtu wa kusimama pale mbele na kusumbua mabeki wa timu pinzani,” alisema kocha huyo.

Simba kesho itaendelea na mazoezi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo imejipanga kurudisha heshima yake kwa kutwaa ubingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles