28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Donbosco Lioness, Vijana Queens vitani leo

Sharifa Mmasi, Mtanzania Digital

HATUA ya nusu fainali ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), imepangwa kuendelea leo jioni kwa michezo miwili kuunguruma ambapo, mtanange wa kwanza utazikutanisha timu za wanawake Donbosco Lioness dhidi ya Vijana Queens.

Baada ya mchezo huo, kikosi cha wanaume timu ya ABC nacho kitashuka dimbani kuumana na wapinzani wao Ukonga Kings wakikutana  kwa mara ya pili kwenye nusu fainali hiyo yenye jumla ya mechi tano (Best of five).

Katika ligi hiyo, mchezaji wa ABC Enerico Maengela ndiye anaongoza kwenye msimamo wa ufungaji akiwa na pointi 175, ambazo hazijafikiwa na yeyote.

Mchezaji anayefuata ni Hajji Mbegu ameifungia klabu yake jumla ya alama 169 wakati Leek Deng akishika namba tatu kwa pointi 157 wote wakitokea katika klabu ya Ukonga Kings.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles