Des Moines, Marekani
BENDI ya muziki wa Injili nchini Marekani, Vijana Wenye Nguvu, imeachia albamu yake fupi (EP) inayofahamika kama Shusha Roho Wako inayopatikana duniani kote kwenye mitandao ya kusikiliza na kupakua muziki.
Akizungumza na Mtanzania Digital mmoja ya waimbaji wanounda bendi hiyo, Diedonne amesema Vijana Wenye Nguvu wametoa EP hiyo ikiwa na nyimbo nzuri tano zenye mguso wa kipekee kwa yeyote atakayesikiliza.
“Bendi yetu inaundwa na vijana watatu ambao ni Dieudonne, Fidel na M’mewa sasa tumetoa EP yetu mpya inayokwenda kwa jina la Shusha Roho yenye nyimbo nzuri zenye upako kama vile Shusho Roho Wako, Niongoze, Wandi Pasa Malo, Nasema Asante na Mwite Yesu ambayo sasa inapatikana kwenye platforms zote za muziki,” amesema Dieudonne.
Aidha, aliongezwa kwa kuwaomba wapenzi wa muziki huo wawatafute kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na YouTube kwa jina la Vijana Wenye Nguvu huku wakiishuskuru studio ya Heaven Music Studio chini ya prodyuza Pasa.