22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Djokovic bado haelewi Australian Open

NEW YORK, Marekani

MKALI wa mchezo wa tenesi duniani, Novak Djokovic, hajafanya uamuzi wa kushiriki au kuiacha michuano ya Australian Open inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari, mwakani.

Hatua hiyo ya Djokovic kubaki njiapanda inatokana na kile waandaaji walichoeleza kuwa hakuna mchezaji atakayetia mguu kwenye mashindano hayo bila kupata chanjo ya Corona.

Mbali ya Mserbia huyo, pia mshiriki mwenzake waliyekutana fainali msimu uliopita wa michuano hii, Daniil Medvedev, naye hajafanya uamuzi wowote, licha ya kwamba ni miezi miwili tu imebaki.

Ifahamike kuwa Djokovic mwenye umri wa miaka 34 ndiye bingwa mtetezi baada ya kumtungua Medvedev kwa seti 7-5 6-2 6-2 walipokutana fainali msimu uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles