27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Mashabiki wavamia uwanjani, wataka kuing’oa VAR

RIO, Brazil

KATIKA sekeseke lililotokea jana, mashabiki wa vigogo wa soka la Brazil, Gremio, waliingia uwanjani na kujaribu kuing’oa mitambo ya teknolojia ya kumsaidia mwamuzi kwa msaada wa marudio ya video (VAR).

Katika mtanange huo dhidi ya Palmeiras, mashabiki hao walivurugwa baada ya timu yao kutandikwa mabao 3-1, licha ya kwamba walikuwa na nafasi ya kushinda baada ya kuongoza bao 1-0.

Huku kikosi chao kikiwa na mastaa waliowahi kupita Bayern Munich, Douglas Costa na Rafinha, mashabiki wa Gremio walihisi penalti mbili walizopata Palmeiras ni ubabaishaji wa VAR.

Ikiwa imebakiza mechi 11 pekee, kichapo walichopata kimewaweka nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Brazil (Serie A), hivyo kuwa kwenye hatari ya kushuka daraja.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,451FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles