Derulo atoka na demu wa 50 Cent

0
837

DeruloNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa sauti kwenye nyimbo za RnB nchini Marekani, Jason Derulo, ameweka wazi kwamba anatoka kimapenzi na Daphne Joy, ambaye amezaa na 50 Cent.

50 Cent, alifanikiwa kupata mtoto wa kiume na mwanamitindo huyo, ambapo walimpa jina la Sire , lakini mrembo huyo inasemekana kuwa anatoka na Derulo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Derulo aliweka picha akiwa na mrembo huyo na kisha kuandika maneno kwamba, “nimepata mpenzi mpya ambaye alifanikiwa kupata mtoto na 50 Cent, lakini kwa sasa nipo naye,” aliandika Derulo.

Hata hivyo, inasemekana kuwa wasanii hao kwa sasa wapo katika mgogoro mkubwa kwenye mitandao ya kijamii hata kabla ya Derulo kuweka wazi kuwa anatoka na mrembo huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here