25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Kylie Jenner ajipeleka kwa ASAP

kylie-jennerNEW YORK, MAREKANI
KUTOKANA na mgogoro unaoendelea kati ya mkali wa hip hop nchini Marekani, Tyga na mpenzi wake, Kylie Jenner, hatimaye mrembo huyo amejipeleka kwa ASAP Roky.

Kuna taarifa zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba wawili hao wamekuwa na mgogoro katika uhusiano wao, huku mrembo huyo akidai kwamba mpenzi wake anaonekana kuwa na mawasiliano na mpenzi wake wa zamani ambaye alizaa naye, Blac Chyna.

Kutokana na hali hiyo, mrembo huyo juzi alionekana akiwa na nyota wa hip hop, ASAP Rocky, wakiwa wanatoka kwenye kumbi za starehe.

Kupitia akauti ya Instagram ya msichana huyo aliandika: “Ninatamani kuwa kwenye uhusiano na ASAP,” aliandika Kylie.

Ujumbe huo umewafanya watu wengi kushangaa huku wakijiuliza kuna nini kati yake na mpenzi wake Tyga? Hata hivyo, sio mara ya kwanza wawili hao kutishia kuachana lakini bado wanadumu pamoja.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles