24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

DCI asisitiza nchi iko salama

Na JANETH MUSHI

-ARUSHA

MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, amesema hali ya ulinzi na usalama nchini ni shwari, kwa kuwa hata makosa ya unyang’anyi yamepungua.

Pamoja na hayo, DCI Boaz amesema hawataacha kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaobainika kujihusisha na masuala ya ujangili, kwani kupitia kikosi maalum kinachoundwa na vyombo vya dola nchini, kimeweza kusaidia kupunguzwa kwa matukio ya ujangili.

“Kwa ujumla, nchi yetu inaendelea kuwa shwari, shwari sana na katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka, hali ya uhalifu imepungua ukilinganisha na robo ya kwanza ya mwaka jana.

“Katika kipindi cha mwaka jana, makosa makubwa katika kipindi cha robo ya kwanza yalikuwa 14,866 na mwaka huu katika kipindi kama hicho kuna makosa 14,355, sawa na upungufu wa asilimia 3.4.

“Hata unyang’anyi wa kutumia silaha umepungua kwa asilimia 4.7, kwani mwaka jana yaliripotiwa makosa 6,897 na mwaka huu yameripotiwa makosa 6,573.

“Kwa hiyo, napenda kuwafahamisha kuwa, huko nyuma tulikuwa na makosa mengi ya ujangili, lakini kwa juhudi ambazo zimefanywa baina ya vyombo vya dola na taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, tumetengeneza timu maalumu kwa ajili ya kupambana na ujangili.

“Kutokana na umoja wetu huo, tumeweza kudhibiti kwa kiasi kikubwa ujangili nchini, tumekamata mitandao, tumekamata silaha zao na nyara na tunajivunia sasa tunakwenda vizuri.

“Pamoja na jitihada hizo, kuna wenzetu wachache katika taasisi mbalimbali ambao wanashirikiana na majangili, wanaendelea kuhujumu juhudi hizo,” alisema DCI.

Kuhusu malalamiko ya ucheleweshaji wa upelelezi katika matukio mbalimbali, alisema baadhi ya mazingira ya kesi yanachangia kuchelewa kwa upelelezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles