23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kampeni ya elimu yazinduliwa Kibaha

Na GUSTAPHU HAULE

-PWANI

MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama, amezindua kampeni maalumu ya Elimisha Kibaha, inayolenga kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 65.

Mshama alizindua kampeni hiyo juzi mjini Kibaha, katika mkutano wa pamoja na wawekezaji wa viwanda, wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa maendeleo.

“Pamoja na uzinduzi wa kampeni, lengo la mkutano ni kujadili changamoto katika sekta ya uwekezaji.

Alisema kuwa, Serikali ya awamu ya tano imetoa kipaumbele cha kutoa elimu bure, hali ambayo imesababisha kuwapo kwa ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiandikisha kwenda shule na hata wanaofaulu kujiunga na kidato cha kwanza.

Alisema kuwa, katika kipindi cha mwaka 2017, wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza walikuwa 3,560, wakati 2018 walikuwa 3,938 na mwaka 2019 idadi hiyo ilizidi kuongezeka mpaka kufikia 4,930.

“Kuwapo kwa ongezeko hilo kumesababisha pia upungufu wa madarasa ya wanafunzi wanaojiandikisha kidato cha kwanza na hata wale wa shule za msingi.

“Leo nazindua kampeni hii kwa ajili ya kuhamasisha michango ya ujenzi wa madarasa katika wilaya yetu.

“Kwa hiyo, nawaomba ndugu zangu wadau na wawekezaji, tushirikiane ili tuweze kufikia malengo na michango inaweza kuwa saruji, kokoto, mchanga, tofali na hata nondo.

“Kufanikishwa kwa kampeni hiyo, kutakuwa chachu ya maendeleo ya elimu wilayani Kibaha, kwa kuwa wanafunzi wote wanaofaulu watakuwa wanapata nafasi ya kusoma bila kuwa na kisingizio cha kukosa nafasi.

“Kwa hiyo, ili tufanikishe mkakati wetu, nawaomba wadau wa maendeleo wajitokeze kwa wingi katika kuchangia kampeni hiyo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles