24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DC atahadharisha ulaji pipi safarini

candyNa BENJAMIN MASESE

MKUU wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, amewatahadhirisha wananchi kutodhubutu kupewa pipi na mtu yeyote ndani ya gari binafsi au basi la abiria.

Amesema  baadhi ya pipi hizo hupakwa dawa za kulevya na kusababisha kupoteza fahamu.

Amesema tayari madhara ya ulaji wa pipi yalimkuta mtumishi mmoja wa Serikali ambaye alipewa pipi ndani ya basi na kujikuta akizinduka akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekeo Toure, akipatiwa matibabu.

Tahadhari hiyo aliitoa alipozungumza na wananchi wa Kata za Igoma na Kishili kuhusu  mambo mbalimbali ya ulinzi na usalama ndani ya wilaya ya Nyamagana.

Tesha ambaye hakutaka kutaja jina lake la mtumishi huyo aliyekula pipi lakini alidokeza cheo chake kuwa ni mkurugenzi.

Alisema  alipewa pipi na abiria mwenzake aliyekuwa jirani na muda mfupi alisinzia na kupoteza fahamu.

“Naombeni wananchi tuwe na tahadhari sana juu ya ulaji wa vitu  ndani ya vyombo  vya usafiri, hili nalisema wazi kwani limekuwa likijitokeza.

“Hivi karibuni kuna mtumishi mmoja alikuwa anasafiri  ambako alipopewa pipi na abiria mwenzake kumbe ilikuwa imepakwa dawa za kulevya.

“Mtumishi huyo ambaye tena ni mkurugenzi alijikuta akizindukia Sekeo Toure, hajui alifikishwa vipi katika hospitali hiyo.

“Epukeni ulaji wa pipi pia kwa sababu umekuwapo   utapeli kwa njia ya simu nao umeendelea kutikisha nchi na watu kuibiwa mamilioni ya fedha,”alisema.

Tesha alizungumzia  suala la wana wanafunzi  waliofaulu  mtihani  wa darasa la saba akiwaonya wazazi  watakaoshindwa kuwapeleka kuanza kidato cha kwanza watafikishwa mahakamani.

Alisema ifikapo Januari 31, 2017 ataanza ziara ya kutembelea shule zote ndani ya Nyamagana  kubaini wanafunzi walioshindwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza na kuwachukulia hatua wazazi wao.

Wananchi wa Igoma na Kishili walimweleza DC  kwamba   kumekuwapo na kero ya kukatika daraja la Fumagila linalounganisha wilaya za Misungwi na Nyamagana na kusababisha wananchi kushindwa kwenda shule hasa   mvua inaponyesha.

Akitoa majibu, alisema tayari Serikali imetenga Sh milioni 300 kwa ajili ya kujenga daraja la Fumagila na kuwataka wazazi kuwasindikiza wanafunzi na kuwavusha upande wa pili  mvua inaponyesha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles