31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali iwasaidie kweli waathirika wa tetemeko Kagera

waathirika-wa-tetemeko-kageraTUNASEMA tangu mwanzo kuwa hii si sahihi hata kidogo, kwamba misaada yote iliyotolewa na taasisi na watu mbalimbali kwa ajili ya madhara yaliyotokana na tetemeko mkoani Kagera hivi karibuni kuwa ni mali ya Serikali na taasisi zake.

Tunasema si sahihi na ndiyo maana siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu, kuwaambia wananchi walioathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo, kuwa wajitegemee wenyewe; kwamba misaada yote iliyotolewa ni ya Serikali na taasisi zake tu, kauli hiyo imewashangaza na kuwashitua viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, miongoni mwa watu wengi mbalimbali.

Katibu wa Taifa wa chama hicho, Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Janeth Rithe, amesema kauli hiyo haikubaliki kwani inadhalilisha waathirika na taasisi zote zilizojitokeza kwa ajili ya kuwasaidia waathirika hao.

Kwamba kauli hiyo ni tangazo bovu linalokosa uaminifu wa mali za wananchi zilizotolewa na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo; na inadhalilisha waathirika wa tetemeko la ardhi.

Ikumbukwe kuwa tangu tetemeko hilo lilipotokea, taasisi na wananchi mbalimbali walijitokeza kuwasaidia waathirika hao.

Tunakumbusha kuwa haileweki watu wanaposhindwa kupewa misaada na badala yake zinatoka kauli kama hizo. Ni busara ya kawaida kuwa hatua ya kwanza katika kushughulikia maafa ni kurudisha hali ya maisha ya watu katika hali ya kawaida sambamba na ukarabati wa miundombinu.

Kwamba suala la ujenzi wa miundombinu ya taasisi za umma, ni jukumu la msingi la Serikali ambalo haiwezi kulikwepa.

Kwamba Serikali ijitenge na kufuta kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa sababu inaweza kusababisha migongano kati ya wananchi na Serikali yao.

Kwamba Serikali inapaswa bila kukwepa kuelekeza misaada iliyotolewa, ikiwamo michango, kwa waathirika wa tetemeko hilo kama ilivyokusudiwa.

Tunapenda kukumbusha taasisi za kiraia nchini kuendelea kuikumbusha Serikali wajibu wake wa msingi wa kuboresha maisha ya watu.

Septemba 10, mwaka huu kulitokea tetemeko la ardhi katika eneo la Kanda ya Ziwa, hususan mkoa wa Kagera ambalo lilisababisha baadhi ya wananchi kufariki na wengine kulazwa, huku nyumba na mali zao zikiharibika vibaya.

Takwimu zilizotolewa na mkuu wa mkoa huo zilionyesha kuwa watu 117,721 waaliathirika kwa kupoteza makazi yao, nyumba 2,072 za makazi zilianguka na 14,595 zilibomoka, baadhi zilipata nyufa hivyo kuzifanya kuwa hatarishi kwa makazi ya binadamu.

Kutokana na hali hiyo, taasisi mbalimbali, pamoja na nchi marafiki, waliitikia wito wa kuwasaidia waathirika wa maafa na kukarabati miundombinu iliyoharibika.

Hadi kufikia Oktoba, mwaka huu, fedha, vyakula na vifaa mbalimbali vya ujenzi vilikuwa vimepatikana kwa njia ya michango mbalimbali.

Tunasema misaada hii ni vizuri ikagawiwa kwa watu wote walioathirika kiasi cha kuwawezesha kurejea kwenye maisha yao ya awali.

Tunadhani shughuli hii ifanywe sambamba na kukarabati taasisi zilizoathirika, na pia miundombinu iliyoharibika.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles