28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Dani Alves adai Messi hana nidhamu

RIO, BRAZI

NAHODHA wa timu ya taifa Brazil, Dani Alves, amedai mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi hana nidhamu kutokana na kauli yake kuwa michuano ya Copa America imejaa rushwa.

Messi aliitoa kauli hiyo mara baada ya Argentina kuondolewa kwenye michuano hiyo ya Copa America dhidi ya Brazil katika hatua ya nusu fainali kwa kichapo cha mabao 2-0.

Messi alionekana kuwatupia lawama waamuzi wa michuano hiyo kwa madai kushindwa kutumia mfumo wa VAR katika baadhi ya makosa ambayo Argentina walikuwa wanafanyiwa dhidi ya Brazil.

Hata hivyo baada ya Argentina kuondolewa, Messi aliendelea kuwalalamikia waamuzi katika mchezo wao wa kumtafuta mshindi wa tatu dhidi ya Chile ambapo Argentina walishinda mabao 2-0, huku Messi akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kugombana na kiungo wa Chile, Gary Medel.

Kutokana na vitendo hivyo, Messi alishindwa kuzuia hisia zake na kuweka wazi kuwa, michuano hiyo imetawaliwa na rushwa, hivyo Alves amedai kauli hiyo ya Messi inaonesha wazi kuwa hana nidhamu.

“Urafiki hauwezi kuwa sawa mara zote kwa kuwa ni marafiki, Messi anaweza kusema kauli hiyo kutokana na kuumia kuondolewa kwenye michuano, lakini kwa upande wangu siwezi kukubaliana naye.

“Kwanza naweza kusema ameonesha kuto kuwa na heshima kwa shirika kama Selecao, kwa maoni yangu ni kwamba Messi amekosa nidhamu hasa kutokana na kiwango chake cha soka duniani, sikutarajia kusikia kauli kama hiyo kutoka kwake.

“Amekuwa rafiki yangu wa karibu kwa kipindi kirefu, tumekuwa tukielekezana ukweli pale tunapokutana, lakini kwa hili ukweli ni kwamba amekosea,” alisema Alves.

Alves na Messi wamekuwa wakicheza pamoja katika klabu ya Barcelona kwa miaka nane kabla ya Alves kuondoka na kujiunga na kikosi cha PSG mwaka 2016, lakini wawili hao wamekuwa na uhusiano wa karibu. Kweney michuano hiyo ya Copa America Brazil wamefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuwachapa Peru mabao 3-1.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles