24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Paul Pogba, Lingard wagombana mazoezini

PERTH, AUSTRAL

KIUNGO wa timu ya Manchester United, Paul Pogba na mchezaji mwenzake Jesse Lingard, jana walipishana kauli wakati wa maandalizi ya mazoezi yao mjini Perth nchini Australia.

Manchester United ipo nchini Australia kwa ajili ya ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu nchini England.

Uongozi wa timu hiyo ulituma video kwenye ukurasa wao wa Twitter ambayo inawaonesha wawili hao wakirushiana maneno huku Lingard akimfuata Pogba na kutaka kumshika shati, ila Victor Lindelof aliwahi kumzuia Lingard.

Kutokana na hali hiyo Pogba alionekana kuchukizwa kwa kiasi kikubwa na kuamua kujiweka pembeni na makundi ya wachezaji jambo ambalo liliacha maswali mengi kwa viongozi na wachezaji wengine kwenye kambi hiyo.

Mashabiki wa Manchester United, walitumia mitandao ya kijamii kulijadili tukio hilo la wachezaji hao huku wengine wakidai Pogba ndio tatizo kubwa kwenye kikosi hicho, hivyo ni vizuri akaachwa aondoke ili wachezaji wengine wawe huru.

Katika kipindi hiki cha kiangazi Pogba amekuwa akihusishwa kutaka kuondoka na kujiunga na mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, hata hivyo timu yake ya zamani ya Juventus inahusishwa kutaka kumrudisha kikosini.

Pogba mwenyewe aliweka wazi kuwa, hana mpango wa kuendelea na Manchester United katika kipindi hiki cha kiangazi, hivyo mashabiki wameshangaa kuona mchezaji huyo anaungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Kikosi hicho cha kocha Ole Gunnar Solskjaer, kiliwasili mjini Perth kikitokea jijini Manchester ambapo kilitumia saa 19.

Katika ziara ya Manchester United kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi, itacheza michezo mbalimbali ikiwa pamoja na Perth Glory, Julai 13, Julai 17 itacheza na Leeds United, huku Julai 20 itacheza dhidi ya Inter Milan, Julai 25 itapambana na Tottenham Hotspur, wakati huo Julai 30 ikipambana na Kristiansund huku mchezo wa mwisho utakuwa Agosti 3 dhidi ya AC Milan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles