27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Nyota 29 watakaoibeba Yanga hadharani

Na Mohamed Kassara-Dar es salaam

KLABU  ya Yanga imeanika kikosi chake cha wachezaji 29, watakaoitumikia msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.

MTANZANIA imeinasa orodha hiyo ya kikosi cha Yanga, ikiwa ni siku moja kabla ya dirisha kwa ajili  usajili wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika  na Kombe la Shirikish Afrika kumalizika.

Wababe hao wa Jagwani wanarejea katika michuano hiyo ya kimaitafa msimu ujao ,baada ya kumaliza nafasi ya pili  msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, hivyo kunufaika na kanuni ya Shirikisho la Soka Afrika(Caf), inayozipa nafasi nne za uwakilishi, nchi ambazo klabu zake zimefanya vizuri katika michuano inayoisimamia, yaani Ligi ya Mabingwa na  Kombe la Shirikisho Afrika.

Tanzania imenufaika na kanuni hiyo, baada ya klabu ya Simba na  Yanga  kufanya vizuri kwa nyakati tofauti katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, Simba ndiyo iliyotoa mchango mkubwa zaidi wa kufanikisha kupatikana nafasi hizo, baada ya kufika robo fainali katika michuano ya Ligi ya mabingwa msimu uliopita ilipotinga robo fainali.

Kikosi kamili cha Yanga msimu ujao kitakuwa na makipa Klaus Kindoki (DRC), Farouk Shikalo(Kenya) na Metacha Mnata ambaye ni mzawa.

 Mabeki, Kelvin Yondan, Andrew Vicent, Juma Abdul, Paulo Godfrey, Ally Mtoni, Ally Ally, Cleofas Sospeter, Muharam Issa Said(wazawa),  Lamine Moro(Ghana) na Moustapha Seleman kutoka Burundi.

Viungo ni Feisal Salum, Mohamed Issa, Juma Mahadhi, Deus Kaseke, Mapinduzi Balama, Gustaph Simon,Raphael Daud,  Abdul aziz Makame, Erick Msigati(wazawa) na Papy Tshishimbi, DRC.

Washambuliaji ni Patrick shibomana,Issa bigirimana(Rwanda),Sadney Ukirthob(Namibia), Maybin Kalengo(Zambia), Juma Balinya(Uganda) na Mrisho Ngassa ambaye ni mzawa.

Baadhi ya wachezaji hao tayari wameanza  kujifua na kikosi cha timu hiyo kilichoko kambini mkoani Morogoro ,chini ya kocha msaidizi, Noel Mwandila.

Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera, pamoja na wachezaji waliokuwa wakizitumikia timu zao za taifa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika(Afcon),wanatarajia kuungana na kikosi hicho baada ya siku 10.

Kwa maana hiyo Yanga imewatema, Pius Buswita, Ramadhan Kabwili ambaye yuko katika majaribio  ya kucheza soka la kulipwa nchini Macedonia , Said Makapu, Haji Mwinyi, Thabani Kamusoko(Zimbabwe) na Gadiel Michael aliyejiunga na Simba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles