26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Curry aongoza kwa mauzo ya jezi NBA

stephen-curryNEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa kikapu wa timu ya Golden State Warrior, Stephen Curry, anaongoza kwa mauzo ya jezi katika michuano ya Ligi ya NBA nchini Marekani.

Mchezaji huyo bora wa tuzo za MVP msimu uliopita, amekuwa na idadi kubwa ya mashabiki na kuifanya jezi yake kuuzika sana sokoni na kuwafunika nyota wengine kama vile LeBron James wa Cleveland Cavaliers na Kobe Bryant wa Los Angeles Lakers.

Mchezaji  huyo amefamnya mauzo makubwa kwa miezi mitatu tangu Oktoba 2015 hadi Desemba mwaka huo huo.

James na Bryant, ambao wanatarajia kustaafu kikapu mwishoni mwa msimu huu, wamekuwa nafasi ya pili na tatu kwa mauzo, wakati nyota wa timu ya New York Knicks, Kristaps Porzingis akishika nafasi ya nne.

Kevin Durant, Derrick Rose, Russell Westbrook, Kyrie Irving, James Harden na Jimmy Butler wameingia katika nafasi 10 za majina yao kuuzika katika jezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles