25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Man United kuongoza mapato duniani

MANCHESTERNEW YORK, MAREKANI

MANCHESTER United huenda ikawa klabu ambayo itaongoza kwa mapato duniani katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

Kwa mujibu wa orodha ya mapato ya klabu iliyotayarishwa na kampuni ya Deloitte ya nchini Marekani, miamba ya nchini Hispania, Real Madrid, kwa sasa wanaongoza kwa mwaka wa 11 kushika nafasi ya kwanza kwa mapato duniani, huku msimu wa mwaka 2014-2015 ilipata euro milioni 577, sawa na pauni milioni 439.

Mabingwa wa Ligi na Klabu Bingwa barani Ulaya, Barcelona, wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na euro milioni 560.8, sawa na pauni milioni 426.6, huku United wakiwa wanashika nafasi ya tatu kwa kujipatia euro milioni 519.5, sawa na pauni milioni 395.2.

Lakini Deloitte wamesema kuna uwezekano mkubwa sana wa United huenda wakawa wamewapita Real Madrid wakati wa kutolewa kwa orodha ijayo.

Manchester United walishuka kutoka namba mbili hadi namba tatu baada ya kushuka kwa mapato yao, lakini Deloitte wanasema ukuaji wa biashara zao, pamoja na uwezo wa kupata mikataba ya thamani kubwa kama ule wa Adidas wa pauni milioni 75, kila mwaka, inasaidia sana klabu hiyo kukuza mapato.

Kutokana na mkataba mpya wa haki za utangazaji katika runinga wa thamani ya pauni bilioni 5.1 utakaoanza msimu wa 2016-17, Real Madrid huenda ikapata tatizo la mapato ya juu.

Ligi Kuu nchini England inaongoza kwa kuwa na klabu nyingi kwenye orodha ya klabu 30 tajiri duniani, ambapo hadi sasa kuna klabu 17 ndani yake. Hali hii inatokana na mikataba mizuri ya utangazaji.

West Ham wamefika kwenye 20 bora kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2005-06, baada ya kupata mapato ya euro milioni 160.9, sawa na pauni milioni 122.4.

Manchester United waliongoza orodha hiyo, ambayo kwa Kiingereza hujulikana kama Deloitte Football Money League, ilipozinduliwa mwaka 1998, walipoandikisha mapato ya jumla ya £87.9m.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles