24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Gerrard ataka Klopp apewe muda

Steven GerrardLIVERPOOL, ENGLAND

NAHODHA wa zamani wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard, ameitaka klabu hiyo kumpa muda kocha wao mpya, Jurgen Klopp, ili aweze kutengeneza timu yake ambayo itaweza kuchukua mataji.

Gerrard anaamini kuwa kocha huyo ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri kama atapewa muda, kwa kuwa ameikuta ikiwa katika wakati mgumu.

Kocha huyo alijiunga na klabu hiyo Oktoba mwaka jana, akitokea Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka mitatu, lakini hadi sasa bado hajaonesha moto wake, hivyo Gerrard ameutaka uongozi wa klabu hiyo kumuamini kocha huyo.

“Nadhani tunatakiwa Klopp kumpa muda, hasa katika kipindi hiki cha usajili na kipindi kile cha maandalizi ya Ligi ili kuweza kuitengeneza timu yake ambayo itacheza kutokana na mifumo yake kwa ajili ya kuleta mataji.

“Kwa upande wangu wala sina wasiwasi na nina furaha kwa kuwa ninaamini Klopp ataweza kukata kiu ya mashabiki wa klabu hiyo.

“Liverpool kwa sasa imekuwa na wakati mgumu wa kuweza kushindana na klabu kama Manchester City na Chelsea, lakini inawezekana kutokana na mifumo ya kocha, kikubwa ni kupewa muda kukaa na wachezaji ambao wanaonekana kuwa na uwezo mzuri,” alisema Gerrard.

Hata hivyo, kocha huyo tangu ameichukua timu hiyo, amefanikiwa kushinda mbele ya vigogo kama vile Chelsea na Manchester City, huku akitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Arsenal na kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo kuwa na amani na timu yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles