27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Pereira ataka kuondoka Manchester United

Andreas-Pereira-615146MANCHESTER, ENGLAND

KIUNGO wa klabu ya Manchester United, raia wa Brazil, Andreas Pereira, amedai kwamba anakosa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza katika klabu hiyo, hivyo ni muda wake wa kuondoka.

Mchezaji huyo amedai kwamba, kutokana na kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi, kutampa wakati mgumu wa kushiriki michuano ya Olympinki mwaka huu nchini Brazil.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye anacheza katika nafasi ya kiungo, hadi sasa amefanikiwa kucheza michezo tisa tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Old Trafford akitokea PSV mwaka 2014.

“Kwa sasa mimi ni mchezaji wa Manchester United, nimesikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari vikitoa taarifa kwamba kuna baadhi ya klabu zinanihitaji, lakini sijui kama United itanitoa kwa mkopo, lakini ninajitahidi ili kuweza kupata nafasi ila Manchester yenyewe itaamua,” alisema Pereira.

Nyota huyo ambaye alitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 mwaka jana kwenye michuano ya Kombe la Dunia, amedai kwamba anatamani kuivaa tena jezi ya Taifa katika michuano mingine.

“Ninajituma sana United, ni wazi kwamba lengo ni kucheza zaidi katika timu ya Taifa, lakini nakosa nafasi ya kutosha chini ya Van Gaal, kitu ambacho kinanipa wakati mgumu wa kuendelea kuwa hapa,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles