26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Cori Gauff aishangaza tena dunia

LONDON, ENGLAND

NYOTA wa tenisi mwenye umri mdogo kutoka nchini Marekani, Cori Gauff maarufu kwa jina la Coco, ameishangaza tena dunia baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya michuano mikubwa ya Wimbledon.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15, ameingia kwenye hatua hiyo baada ya kumgalagaza mpinzani wake Polona Hercog kwa seti 3-6, 7-6, 7-5 huko jijini London nchini Uingereza.

Dunia ilianza kushangaa baada ya kumuona msichana huyo akipangiwa kucheza na bingwa mara tano wa Wimbledon, Venus Williams katika raundi ya kwanza ya mashindano hayo, lakini kitu cha ajabu ni kwamba binti huyo aliweza kushinda na kumuondoa bingwa huyo kwenye michuano.

Coco alionesha kiwango hicho mbele ya mama yake Candi na baba yake Corey, ambao walionekana kumsapoti kila wakati hadi anashinda mchezo huo.

Corey aliwahi kuwa nyota wa zamani wa mchezo wa kikapu katika timu ya Georgia State University, wakati huo mama yake Candi alikuwa katika timu ya Florida University. Lakini hawakuwahi kufikiria kama mtoto wao huyo ataweza kufanya makubwa kwenye Wimbledon.

Coco anatajwa kuwa msichana wa kwanza mwenye umri mdogo kuweza kufuzu hatua ya 16 bora ya Wimbledon baada ya kufanya hivyo na Jennifer Capriati mwaka 1991 ambapo alikuwa na umri wa miaka 14.

“Huu ulikuwa ni mchezo wangu wa kwanza kucheza kwenye kiwacha cha kati, sikuwahi kuwa na ndoto ya kufanya hivi, lakini kila nikiwa uwanjani najipa imani kuwa ninaweza kufanya lolote hata kama mpinzani ameanza kutangulia kufanya vizuri.

“Haikuwa kazi rahisi kufikia hatua hii, ushindani ni mkubwa changamoto ni nyingi, lakini ninashukuru kila siku ninazidi kupambana kwa ajili ya kutaka kutimiza malengo yangu, ninaamini hakuna kinachoshindikana, kikubwa ni kujituma kufanya mazoezi kwa nguvu,” alisema Coco.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles