22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

FIFA kuongeza timu 32 Kombe la Dunia wanawake

ZURICH, USWIS

RAIS wa shirikisho la soka la kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ameweka wazi kuwa wapo kwenye mpango wa kuongeza timu kufikia 32 kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa wanawake.

Mbali na kuongeza idadi ya timu pia wanatarajia kuongeza na thamani ya zawadi kwa mshindi ambapo atachukua mara mbili ya kiasi wanacho chukua sasa.

Halmashari ya FIFA kupitia wanachama wake 37, wanatarajia kukutana Machi mwakani kwa ajili ya kupiga kura ya kumchagua mwenyeji wa michuano hiyo mwaka 2023.

Tayari nchi tisa zimeonesha dalili za kutaka kuwa wenyeji wa mashindano hayo, miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na Brazil na Afrika Kusini. Huku Argentina, Australia, Bolivia, Colombia, Japan, New Zealand na South Korea zimetakiwa kuanza kurekebisa miundo mbinu ya michezo kwa ajili ya kuwa kwenye orodha ya nchi zitakazo jadiliwa juu ya kuwa mwenyeji.

“Lazima zoezi hili lifanyike mapema kwa ajili ya kuona uwezekano wa kuongeza timu kufikia 32 kuanzia mwaka 2023, tutafanya majadiliano ya mapema ili kufikia makubaliano juu ya zoezi hilo.

“Wanachama wote wanatakiwa kutoa mawazo yao juu ya suala hilo ili kuhama kwenye timu 24 hadi kufikia 32,” alisema Infantino.

Hii sio mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kuongezeka timu, ilianza mwaka 1991 ambapo timu zilikuwa 12 tu, lakini mwaka 1999 zikaongezeka hadi kufikia timu 16, lakini baada ya kufikia mwaka 2015 zikaongezeka tena hadi kufikia timu 24.

Infantino aliongeza kwa kusema, endapo watafanikiwa kuongeza na kufikia timu 32 yatakuwa mafanikio makubwa sana hasa katika kukua kwa soka.

“Hakuna kisicho wezekana hasa katika mafanikio ya michuano ya Kombe la Dunia kwa wanawake, lazima tuamini kwenye vitu vikubwa na kuja kufanya kama tulivyofanya miaka ya nyuma, sasa ni wakati wa kufanya hivyo kwa timu za wanawake,” aliongeza.- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles