28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Veta Kihonda yabuni teknolojia ya kuongoza magari

Na Christina Gauluhanga, Dar es Salaam

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), Chuo cha Kihonda,  Morogoro kimebuni mfumo mpya wa kieletroniki wa kuongoza magari ambao utawasaidia askari kuepuka kugongwa mara kwa mara.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Julai 7, katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba (DITF), Mwalimu wa madereva wa magari makubwa  kutoka VETA Kihonda, Wilium Munuo amesema mfumo huo humsaidia askari kuongoza magari akiwa pembeni ya barabara.

Amesema anachokifanya askari huyo ni kutumia mfumo huo kuruhusu magari yapite kwa utaratibu maalum.

“Mfumo huu ni Muhimu hapa nchini kwetu ambao umemebuniwa na wanafunzi pamoja na walimu kwakuwa askari huweza kuongoza taa akiwa amekaa pembeni,” amesema.

Amesema pia chuo hicho kinaendelea kuratibu shughuli mbalimbali ikiwamo ubunifu wa bidhaa nyingine ili wanafunzi waige.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles