Na Mwandishi Wetu
Marais wa China na Ufaransa wamefikia mapatano ya kibiashara ya thamani ya mabilioni ya Euro baada ya mazungumzo yao mjini Paris.
Rais Emmanuel Macron wa Ufarasa na Rais Xi Jinping wa China walitiliana saini mapatano hayo ya kibiashara hapo jana.
Licha ya upinzani wa Rais Macron dhidi ya mradi mkubwa wa ujenzi wa miundombinu wa China wenye lengo wa kuyaunganisha mabara ya Asia na Ulaya, Rais huyo amempokea kiongozi wa China anayefanya ziara barani Ulaya.
Bwana Macron pia amesem kuwa kampuni ya AirBus imetia saini kuiuzia China ndege 300 za Abiria. Ufaransa na China pia zimetiliana saini mikataba ya nishati, usafirishaji pia katika sekta ya chakula.
Hata hivyo maafisa wametahadharisha kwamba nchi za Umoja wa Ulaya zinaweza kuwa tegemezi kwa vitega uchumi kutoka China.