31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

CHINA, UFARANSA, ZATILIANA SAINI MKATABA WA MABILIONI YA FEDHA

Na Mwandishi Wetu

Marais wa China na Ufaransa wamefikia mapatano ya kibiashara ya thamani ya mabilioni ya Euro baada ya mazungumzo yao mjini Paris.

Rais Emmanuel Macron wa Ufarasa na Rais  Xi Jinping wa China walitiliana saini mapatano hayo ya kibiashara hapo jana.

Licha ya upinzani wa Rais Macron dhidi ya mradi mkubwa wa ujenzi wa miundombinu wa China wenye lengo wa kuyaunganisha mabara ya Asia na Ulaya, Rais huyo amempokea kiongozi wa China anayefanya ziara barani Ulaya.

Bwana Macron pia amesem kuwa kampuni ya AirBus imetia saini kuiuzia China ndege 300 za Abiria. Ufaransa na China pia zimetiliana saini mikataba ya nishati, usafirishaji pia katika sekta ya chakula.

Hata hivyo maafisa wametahadharisha kwamba nchi za Umoja wa Ulaya zinaweza kuwa tegemezi kwa vitega uchumi kutoka China.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles