28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

CHAGONJA, WENZAKE KUAGWA LEO POLISI

Na Mwandishi Wetu

-DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja na wenzake Hamdani Omari Makame na Kenneth Kasseke, wanatarajiwa kuagwa leo baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Chagonja, Hamdani ambaye alikuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar na Kasseke wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya wamefikia umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria kwa kutimiza miaka sitini katika utendaji wao wa kazi Julai mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, hafla ya kuwaaga wastaafu hao itafanyika leo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam kuanzia saa moja  asubuhi.

“Katika utumishi wao uliotukuka ndani na nje ya Jeshi la Polisi, walishika nyadhifa mbalimbali na kuliletea sifa Jeshi la Polisi ndani na nje ya nchi. Kama tunavyofahamu kuwa uhalifu hauna mipaka, wameshiriki kikamilifu katika operesheni mbalimbali za kitaifa, kikanda na kimataifa.

“Kutokana na mchango wao kwa taifa, wametakiwa kuendelea kuwa msaada kwa Jeshi la Polisi wakati wowote watakapohitajika kutoa ushirikiano wa namna yoyote ili kusaidia kupunguza uhalifu hapa nchini kwa sababu suala la usalama ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine, na taaluma hiyo wanayo watu wachache.

“Tunaamini watakuwa mabalozi wa Jeshi la Polisi Tanzania, hususani katika kipindi hiki cha ushirikishwaji wa wananchi katika suala la ulinzi na usalama nchini, mahali popote watakapokuwa wakiendelea na shughuli zao za kila siku baada ya kustaafu,” alisema Mwakalukwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles