26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA SCOPION YAPIGWA KALENDA TENA

Na FARAJA MASINDE

-DAR ES SALAAM

KESI ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete (34) maarufu ‘Scorpion’, katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, imeahirishwa hadi Agosti 24, mwaka huu.

Hakimu Mkazi Flora Haule kwa kuongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga, aliahirisha kesi hiyo jana baada ya Wakili wa utetezi, Juma Nassor kushindwa kuhudhuria mahakamani.

“Kufuatia wakili wa upande wa utetezi kushindwa kuhudhuria mahakamani, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea kusikiliza kesi ndogo kwa upande wa waleta maombi kwa kuwa upande wa Jamhuri tayari tumefunga ushahidi,” alisema Wakili Katuga.

Kufuatia maombi hayo, Hakimu Flora alihairisha kesi hiyo na kupanga kusikilizwa Agosti 24, mwaka huu.

Kesi hiyo imefikia uamuzi huo kufuatia upande wa utetezi kufuangua kesi ndogo ukidai kuwa Scorpion alilazimishwa kutoa maelezo kwa nguvu wakati akihojiwa katika Kituo cha Polisi Buguruni jambo lililopingana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na hivyo kuibua kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Katika ushahidi uliotolewa Agosti 8, mwaka huu, shahidi wa tisa ambaye ni DC Bryson, alisema kuwa alifanya mahojiano na Scorpion kwa huru na amani, huku mtuhumiwa huyo akikiri kosa la kujeruhi na kukana kosa la wizi.

“Septemba 12, 2016 mtuhumiwa alifika Kituo cha Polisi Buguruni akiwa na marafiki zake wawili ambao ni Hussein Fundi na Deus maarufu ‘Pamba Kali’, baada ya kupewa idhini na mkuu wa upelelezi nilichukua maelezo ya mtuhumiwa kufuatia tuhuma zilizokuwa zikimkabili za kujeruhi na unyang’anyi,” alisema.

Katika hati ya mashtaka, ilidaiwa kuwa Septemba 6, mwaka huu saa 4 usiku, maeneo ya Buguruni Sheli, Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, aliiba cheni ya silva yenye uzito wa gramu 34, ikiwa na thamani ya Sh 60,000, black bendi ya mkononi na fedha taslimu Sh 330,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh 474,000 mali ya Said Mrisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles