22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema ‘feki’ waibuka tena

??????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????? NA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM

WATU kadhaa jana walikamatwa wakijaribu kufanya maandamano katika eneo la Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumpinga mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa.

Tukio la kukamatwa kwa watu hao lilitokea baada ya kubainika hawakuwa wanachama wa Chadema bali walitumwa na watu ambao hawajafahamika kwenda kufanya fujo katika ofisi hizo.

Wakizungumza na gazeti hili watu walioshuhudia tukio hilo walisema lilitokea saa 5.30 asubuhi ambapo walinzi wa Chadema waliwadhibiti waandamanaji watano na kuwahifadhi katika moja ya vyumba vya ofisi za makao makuu.

Walisema miongoni mwa waliokamatwa na kuwekwa kwenye ofisi hizo ni pamoja na waandishi wa habari wawili waliokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kazi.

MTANZANIA Jumamosi lilifika ofisi za Chadema na kuthibitishiwa na maofisa wake kuwa walinzi wake waliwakamata waandishi wa habari, akiwemo mpiga picha wa kampuni ya Uhuru Publication (UPL), Christopher Lissa na mwenzake aliyetambuliwa kwa jina moja Mathew anayefanya kazi katika kituo cha Televisheni cha Star.

“Walifika watu hapa wasiozidi ishirini wakiwa wamevaa fulana za chama pamoja na kubeba mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kumpinga mgombea urais wa Chadema. Walipofika eneo la ofisi walizuiliwa lakini walikaidi ndipo baadhi ya maofisa wa usalama wa chama walilazimika kuingilia kati kwa kuwakamata watu watano wakiwemo waandishi wawili na kuwafungia katika ofisi za Chadema.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo, Lissa alidai kuwa alikuwa akifuatana na waandamanaji hao lakini alikuwa akitimiza wajibu wake wa kikazi baada ya kupewa taarifa kuwapo kwa maandamano hayo juzi.

Alisema alikutana na waandamanaji hao eneo la Kinondoni Manyanya ambako walikubaliana kukutana na walikwenda na gari kabla ya kushuka walichukua fulana na kuvaa kisha waliteremka wakiwa na mabango na kuanza kuandamana.

“Nilifika tangu saa tatu asubuhi eneo la Manyanya kwa ajili ya kupiga picha watu, lakini wakati nawapiga picha tulipofika karibu na ofisi za Chadema wakaanza kutupiga,” alisema Lissa.

Alisema baada ya vurugu hizo walikamatwa kwa nguvu na kuingizwa katika ofisi za Chadema huku wakiendelea kupigwa.

Alisema baada ya kuona hali imekuwa mbaya alijaribu kutoroka kwa kupanda ukuta uliowekwa uzio na kushindwa hali iliyomfanya kutokwa na damu baada ya kukatwa na waya za uzio.

Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru, Ramadhani Mkoma, wamelaani kitendo cha mwandishi huyo kupigwa huku wakitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua waliohusika kufanya kitendo hicho.

“Tunalaani vikali kitendo hicho kilichofanywa na kundi la maofisa na walinzi wa chama hicho kuingilia uhuru wa vyombo vya habari, wamefanya unyama huo dhidi ya mwandishi wetu,” alisema Mkoma.

Alisema wanasikitishwa na kitendo cha Chadema kuamua kufanya siasa chafu zinazohusisha harakati zao ambazo zimeshindwa kufanikisha kuwashawishi Watanzania ili wawachague.

Alisema wanaamini vyombo vya habari vitakemea tukio hilo pia hatua stahiki kwa vyombo vya dola ikiwemo polisi vitachukua hatua dhidi ya waliohusika na unyama huo.

Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, alilifananisha na matukio ya kutengeneza watu na kufanya maandamano kama mbinu chafu na dalili za kushindwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kudai kuwa chama hicho kwa sasa kimezidiwa na kasi ya mabadiliko kutokana na kuendelea kuhujumu Ukawa.

“Hii CCM ambayo imezidiwa na wakati wa mabadiliko, imefanya mikakati ya kipuuzi kuonyesha upuuzi wao tulipata taarifa kuwa wamekaa vikao Kurasini na kuwapa watu kadi na tshirt (fulana) ili waandamane kwa bahati mbaya hawajafanikiwa,” alisema Mnyika.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles