22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Msikiti wa Makka waanguka, waua 65

makkah1MAKKA, SAUDI ARABIA

MSIKITI Mkuu wa Makka ambao waumini wa dini ya kiislamu wamekuwa wakiutumia kufanyia Hija umeanguka na kuua watu 65 huku wengine wanane wakijeruhiwa vibaya katika tukio lililotokea jana nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC chanzo cha tukio hilo ni winchi lililokuwa linatumika katika ukarabati wa msikiti huo kupata hitilafu na kuangukia jengo la msikiti huo.

Mamlaka za usalama nchini humo zimethibitisha kutokea kwa tukio hilo na taarifa hizo ilizisambaza kupitia mtandao wa tweeter.

Haijafahamika mara moja kilichotokea, lakini picha zilizoonekana kutoka katika eneo la tukio zilionyesha sehemu ya winchi hilo kubwa lenye rangi nyekundu likiwa limeangukia paa la msikiti huo.

Tukio hilo limetokea wakati ambako Waislamu kutoka katika mataifa mbalimbali duniani wakijiandaa kwenda hija. Tukio ambalo linafanywa kwa mwaka mara moja. Maelfu ya watu kutoka katika mataifa mbalimbali walitarajiwa kuwasili katika jiji la Saudi baadae mwezi huu.

Mchambuzi wa masuala ya Kiarabu Sebastian Usher wa shirika la BBC anasema shughuli kuupanua msikiti huo umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles