Celine amuota mume wake

0
772

The Grammy Nominations Concert Live - ShowLAS VEGAS, MAREKANI

MSANII wa muziki nchini Marekani raia wa Canada, Celine Dion, amedai kwamba amekuwa na kipindi kigumu tangu afariki mume wake, Rene Angelil.

Msanii huyo amesema kwamba, tangu Januari 14 mwaka huu alipofariki mume wake amekuwa na kipindi kigumu wakati wa kulala kwa kuwa anamuota mara kwa mara.

“Watu niliokuwa nao karibu ni mume wangu, tangu alipofariki nimekuwa nikimuota huku akiwa na watu hao pamoja katika sehemu mbalimbali za starehe.

“Ndoto hizo zinanifanya niwe na furaha kwa kuwa ninamkumbuka, lakini ninakuwa na wakati mgumu kwa kuwa simuoni kwenye macho yangu,” alisema Celine.

Hata hivyo, msanii huyo amedai kwamba atafanya kitu maalumu kwa ajili ya kumkumbuka mume wake Januari 16 ambapo alitarajia kutimiza miaka 74.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here