Yamoto Band kunogesha uchangiaji damu

0
894

yamoto-b-1024x752NA MWANDISHI WETU

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imepanga kufanya maadhimisho ya utoaji wa huduma ya magonjwa ya dharura na ajali ambayo yanatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Karume (Ilala) yatakayonogeshwa na bendi ya Yamoto.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuanzia Februari 25 hadi 26 yakisindikizwa na kaulimbiu ya ‘Changia Damu Okoa Maisha’.

Mratibu wa tamasha hilo ambaye ni mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, ameomba Watanzania wajitokeze kuchangia damu ili waokoe maisha ya ndugu, marafiki na watu wengine kwa ujumla.

“Ni maadhimisho yenye lengo zuri, tujitokeze kwa wingi kuchangia damu kwa ajili ya watoto wetu, kaka na dada zetu ambao wamekosa damu ya kutosha,” alieleza Shigongo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here