20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Khloe adai yupo ‘single’ kwa sasa

Khloe_KardashianNEW YORK, MAREKANI

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Khloe Kardashian, ameweka wazi kwamba ameachana na mpenzi wake, James Harden na sasa yupo ‘single’.

Mrembo huyo awali alikuwa anatoka na Lamar Odom, lakini walikuja kuachana baada ya Odom kuathirika na dawa za kulevya na ndipo akaamua kuangukia kwenye penzi la Harden ambaye ni nyota wa kikapu wa timu ya Houston Rockets ambayo inashiriki Ligi ya NBA nchini Marekani.

Hata hivyo, Khloe kwa sasa ameonekana kuwa karibu na Odom ambaye ametoka hospitali alipokuwa anapata matibabu baada ya kuzidiwa na utumiaji wa dawa za kulevya.

“Harden ni mtu nilikuwa naye kwa karibu, lakini naomba niwe mkweli kwamba ninaona niishi peke yangu kwa sasa ila nitaendelea kufanya mawasiliano naye,” alisema Khloe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles