28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mourinho athibitisha kumalizana na Man United

MourinhoMANCHESTER, ENGLAND

ALIYEKUWA kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, amewaeleza rafiki zake wa karibu kwamba amemalizana na Klabu ya Manchester United, hivyo ataanza kuitumikia wakati wa majira ya joto mwaka huu.

Kocha huyo amekuwa nje ya uwanja tangu alipofukuzwa na Klabu ya Chelsea Desemba mwaka jana, lakini wiki iliyopita aliweka wazi kwamba amechoka kukaa bila kuifundisha timu hivyo yupo mbioni kurudi viwanjani.

Mourinho amedai kwamba kila kitu kimekamilika hivyo atachukua nafasi ya kocha Van Gaal.

Hata hivyo, Van Gaal bado ana mkataba wa mwaka mmoja katika klabu hiyo ya United, lakini inaonekana wazi kwamba mkataba huo unatarajiwa kuvunjwa ili kumpisha Mourinho afanye kazi yake.

Mwanzoni mwa wiki hii Van Gaal alisema kwamba, hakuna uwezekano wowote wa Mourinho kutua Old Trafford, hizo zote ni habari za kutengenezwa na kudai kwamba hana wasi wasi kwa hilo.

Ujio wa Mourinho katika klabu ya Manchester United utaleta upinzani mkubwa na Manchester City ambapo anatarajia kutua Pep Guardiola akitokea Bayern Munich.

Wawili hao walianza kutofautiana wakati wanafundisha klabu kubwa za nchini Hispania, ambapo Mourinho akiwa Real Madrid huku Guardiola akiitumikia klabu ya Barcelona.

Hivyo makocha hao bora duniani wanatarajia kuanza kazi majira ya joto mwaka huu nchini England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles