22.5 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

West Ham yaitoa Liverpool Kombe la FA

553LONDON, ENGLAND

WAGONGA nyundo wa jijini London, West Ham, wamefanikiwa kuwatoa nje majogoo wa Anfield, Liverpool katika mchezo wa mzunguko wa nne wa Kombe la FA.

West Ham walianza kuandika bao lao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Michail Antonio, katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza baada ya kupokea mpira ambao ulipigwa na Enner Valencia.

Liverpool walifanikiwa kuchomoa bao hilo kupitia kwa kiungo wao Philippe Coutinho kwa mpira wa adhabu na kujaa wavuni moja kwa moja.

Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika huku timu hizo zikiwa zimefungana 1-1, ndipo zikaongezwa dakika 30 ambazo West Ham walizitumia vizuri na kuwaangamiza wapinzani wao kwa bao ambalo lilifungwa na Angelo Ogbonna.

Kutokana na matokeo hayo, West Ham watapambana na Blackburn katika mchezo wa mzunguko wa tano kwenye michuano hiyo ambao utapigwa Februari 21 mwaka huu.

Hata hivyo, baada ya kichapo hicho kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema kwamba amekuwa na wakati mgumu hasa anapopoteza mchezo, lakini anafuraha kuona baadhi ya wachezaji wake wamerudi uwanjani.

“Hakuna ambaye anapenda timu yake ipoteze mchezo kama ilivyo katika baadhi ya michezo yetu, lakini furaha yangu kubwa kuona baadhi ya wachezaji ambao walikuwa majeruhi wamerudi uwanjani kama vile Daniel Sturridge, Philippe Coutinho na Divock Origi,” alisema Klopp.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles