33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yatoa maamuzi magumu

ANDREW MSECHU Na PATRICIA KIMELEMETA – DAR ES SALAAM

HALMASHAURI Kuu Taifa ya CCM (NEC) imetoa maamuzi magumu ya kuwasamehe wanachama waliofukuzwa kwa kuwarudishia uanachama wao, huku kikimweka mmoja katika uangalizi.

Aliyewekwa katika uangalizi ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu kwa muda usiojulikana.

Akiwasilisha maazimio ya kikao cha NEC, baada ya kikao chamaadili na kikao cha Kamati Kuu, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally alisema chama hicho kimeamua kuchukua maamuzi magumu kurejesha mshikamano.

Uamuzi huo ulitolewa katika kikao hicho kilichoanza juzi na kumalizika jana, chini ya uenyekiti wa Rais Dk. John Magufuli.

Alisema kikao hicho kimewarudishia uanachama wanachama wake wanne wa kiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Erasto Kwirasa.

Wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara,Christopher Sanya na aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge.

Dk. Bashiru alifafanua kuwa NEC imeamua kumweka chini ya ungalizi aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Iringa, Msambatavangu ambaye alifukuzwa kwa kosa la maadili.

“Baada ya chama kumfukuza kwa kosa la kimaadil ialilolifanya, Halmashauri Kuu imeamua kumuweka chini ya uangalizi aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu baada ya kuomba kurudishiwa uanachama,” alisema.

Dk. Bashiru alisema pia kuwa NEC imemwagiza aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Uvinza, Zuber Majaliwa kuwasilisha rufaa yake kuanzia ngazi husika wakati adhabu yake ikiendelea.

Majaliwa alisimamishwa uanachama na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Uvinza, huku ikimpa karipio Hasnain Murji kutokana na kukabiliwa na makosa ya kimaadili.

UTEUZI WA WAGOMBEA

Dk. Bashiru alisema katika kikao hicho, NEC imepitisha jina la Abdallah Mtolea kuwa mgombea wa chama hicho katika Jimbo la Temeke.

Mtolea ambaye pia alikuwa mbunge wa Temeke kupitia CUF, alijiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na CCM Oktoba mwaka huu.

Alisema NEC imepitisha majina ya wagombea wa nafas imbalimbali za uongozi ndani ya chama kuanzia wilaya, mikoa na taifa ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi baada ya waliokuwa katika nafasi hizo kupangiwa majukumu mengine ya kiserikali na kufariki.

Alitaja majina ya wagombea hao kwa nafasi ya ujumbe wa NEC kupitia Jumuiya ya Wazazi ni Dk. Damas Kashegu, Asha Feruzi, Galila Ramadhan na Makene Boniphas.

Dk. Bashiru alisema nafasi ya Mwenyekiti wa chama Mkoa wa Iringa ni pamoja na Dk. Abel Mwendawile, Aman Mwamwindi na Sabas Mushi, wakati nafasi ya Katibu, Itikadi na Uenezi Mkoa wa Simiyu ni Mashaka Makongoro, Mayunga Ngokolo na Heri Zebedayo.

Alisema nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Mwanza nipamoja na Bahebe Ezekiel, Nyiriza Makongoro, Masso Jane na Misogalya Kilangi wakati nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya ya Kibaha Vijijini ni pamoja na Amina Kobo, Lemmy Joel na Hamid Shebuge.

Dk. Bashiru alisema NEC imetupilia mbali pingamizizilizowekwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Antony Dialo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Lindi, Aisha Ally, Mjumbe wa NEC, Salim Mohamed na Mwenyekiti wa chama Wilaya ya Ngara, George Rubagora na kuwataka viongozi hao kuendelea na nyadhifa zao kama kawaida.

Alisema halmashauri hiyo pia imeiagiza Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya chama hicho (UVCCM), kurudia mchakato mzima wa kupendekeza majina ya wagombea wa nafasi ya ujumbe wa NEC atakayewakilisha jumuiya hiyo.

Dk. Bashiru alisema NEC imeipongeza Serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa kutekeleza ilani ya chama hicho katika kipindi cha miaka mitatu pamoja na kusimamia kodi na ushuru mbalimbali zinazotolewa.

Alisema lakini pia wameiopongeza Serikali kwa utekelezajiwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), kuboresha usafirishaji wa barabara, reli, majini na nchi kavu, pamoja na kuimarisha uchumi wa nchi.

Waliitaka Serikali kuongeza kasi katika kipindi hiki cha miaka miwili iliyobaki ili waweze kukamilisha mipango yote iliyokusudiwa hadi ifikapo 2020.

HATIMA YA MEMBE

Katika mkutano huo, Dk. Bashiru alikataa kuzungumzia suala la kada wa chama hicho, Bernard Membe ambaye alimwita kuzungumza naye kabla yakufanyika kwa kikao cha NEC kilichomalizika jana.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Dk. Bashiru alisema hawezi kujibu swali lolote linalohusu suala la Membe katika mkutano huo kwa kuwa anatekeleza kile alichotumwa na mwenyekiti wake, kutoa taarifa ya yale waliyokubaliana katika mkutano wa NEC ulioanza juzi na kumalizika jana.

Dk. Bashiru alipokuwa katika mikutano yake mjini Bukombe, Geita Desemba 1, alimwita Membe ambaye pia aliwahi kuwa miongoni mwa waliowahi kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kufuatia taarifa alizodai kuwa zinazagaa katika mitandao ya kijamii, zikieleza nia yake ya kuwania kumpinga Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao.

Alisema tangu alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM hajawahi kuonana wala kuwasiliana na Membe, lakini sasa anachukua uamuzi wa kumwita iliazungumze naye kwa kuwa katika kipindi cha nyuma chama hicho kiliumizwa sana na makundi, fitina, uongo na nguvu ya pesa, mambo ambayo kwa sasa hawezi kuyaendeleza.

Hata hivyo, baada ya kuendelea kwa majibizano na taarifa mbalimbali kutokana na hatua hiyo, Dk. Bashiru alimtaka Membe kufika ofisini kwake kabla ya kikao cha NEC kilichofanyika juzi na jana.

Hata hivyo, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa baada ya hapo, iwapo Membe alionana na Dk. Bashiru au laa, japo kuwa alisema mlango ukowazi kufanya majadiliano maalumu kuhusu mambo mengine ambayo hayahusiani na maamuzi ya NEC jana.

Dk. Bashiru pia alikanusha taarifa zilizokuwa zikizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa mjumbe wa NEC kutoka Mara, Stephen Wassira alizuiwa kuingia katika kikao hicho jana asubuhi.

Alisema Wassira alihudhuria kikao hicho na alikuwa miongoni mwa watu waliochangia kwa kujiamini na alitoa mchango mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles