Vanessa Mdee azindua viatu kwa wanafunzi wa kike

0
2205

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva nchini, Vanessa Mdee amezindua bidhaa zake za viatu maalum kwa wanafunzi hasa wasichana alizozipa jina la ‘Bora Star by Vanessa Mdee’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, leo Jumanne Desemba 18, ametuma ujumbe na picha akionyesha viatu hivyo huku akisema imekuwa ni ndoto yake kwa muda mrefu.

“Ilikuwa ndoto yangu kutengeneza bidhaa itakayonufaisha na kuboresha maisha ya msichanawa kitanzania ama  kiafrika na leo nimetimiza ndoto yangu, nasema asante Mungu,” ameandika Vanessa.

Aidha baada yaVanessa kutuma ujumbe huo wasanii wenzake na mashabiki zake wametoa maoni ya kumpongeza kwa hatua hiyo huku wakimwambia amezindua wakati sahihi maana ni msimu wa wazazi kuwanunulia watoto wao vifaa vya shule kwa ajili ya maandalizi ya mwakani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here