22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Tanga wampiga Nundu kijembe

OSCAR ASSENGA-TANGA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, kimesema wanachama wake wanaosema watagombea Uchaguzi Mkuu wa 2020, wanataka kuwaondoa wenzao katika malengo yao.

Hayo yalisemwa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Shaibu Akwilombe, ikiwa ni siku moja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Omari Nundu, kutangaza azma ya kuwania tena Ubunge wa Tanga mjini mwaka 2020.

Akwilombe alisema malengo yao hivi sasa ni kujikita katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwaka huu ili kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri kama ilivyokuwa chaguzi zilizopita.

 “Nilikuwa safari na taarifa hii sikuiona kwa haraka au kuisikia maana ndio nimefika Tanga jana usiku, hivyo kwangu siwezi kuichukulia kama taarifa rasmi, kanuni za uchaguzi ni jambo linalotawaliwa na ratiba, kwa sasa hatuzungumzii uchaguzi wa 2020, nguvu kubwa sasa ni Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Kufanya hivyo (kutangaza kugombea) ni kufanya kampeni kabla ya wakati, kama yupo mtu anakiuka taratibu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambazo zimekwishatangazwa na chama tutamshughulikia,” alisema.

Akizungumza juzi wakati wa makabidhiano ya vifaa vya Hospitali ya Wilaya ya Tanga inayojengwa eneo la Masiwani, Nundu alisema atawania ubunge wa Jimbo la Tanga mjini mwaka 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles