24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kubaka, kulawiti binti wa miaka 16

AVELINE KITOMARY NA ERICK MUGISHA (DSJ)-DAR ES SALAAM

MKAZI wa Kigogo Kati, Ibrahim Selemani (20), amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka mawili, likiwamo la ubakaji.

Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Aboudi Yusuph, alidai mbele ya Hakimu Frank Moshi kuwa Februari 9, mwaka huu eneo la Kigogo, Wilaya ya Kinondoni, mtuhumiwa alimbaka msichana wa miaka 16.

Katika shtaka la pili mshtakiwa alidaiwa siku hiyohiyo katika eneo hilo, alimwingilia kinyume na maumbile msichana huyo.

Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo huku upande wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Moshi alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria, watakaotoa bondi ya Sh milioni moja kila mmoja.

Hata hivyo, mshtakiwa alirudishwa rumande hadi Julai 15 baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

Wakati huo huo, Hassan Mohamed  (22), mkazi wa Mabibo Luhanga, amepandishwa kizimbani kwa shtaka la kujaribu kubaka.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Anifa Mwingira, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Matarasa Hamisi, alidai Mei 17 eneo la Mburahati, Wilaya ya Kinondoni mshtakiwa alijaribu kumbaka mwanamke mwenye  miaka 27.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Mwingira alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya Sh 50,000.

Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa tena Julai 15.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles