26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Waandamanaji Hong Kong wavamia Bunge, China yataka uchunguzi

Hong Kong, China

BAADHI ya waandamanaji Hong Kong, wamevamia Bunge la nchi hiyo katika maadhimisho ya mji huo kurejeshwa katika utawala wa China mwaka wa 1997, wakati kukiwa na hasira ya umma kuhusiana na sheria ambazo zitaruhusu watuhumiwa kupelekwa China bara kufunguliwa mashitaka.

Maandamano hayo yamekuwa ni hatua ya moja kwa moja ya kuipinga Serikali ya China kuwa na mkono wake katika uendeshwaji wa mji huo wenye mamlaka ya ndani.

Baadhi ya waandamanaji waliingia kwa nguvu kwenye jengo hilo, wakitishia kuvuruga shughuli za Serikali lakini haikufahamika mara moja ni wangapi walibaki ndani.

Maelfu ya wanaharakati wa kidemokrasia walifanya maandamano mengine ya amani, wakimkata kiongozi wa mji huo anayeegemea Serikali ya China kujiuzulu na kubatilisha kile wanachokiona kuwa ni miaka mingi ya kushuka kiwango cha uhuru.

Serikali ya China imelaani kitendo cha kulizingira Bunge la Hong Kong na kusema inaunga mkono kufanyika uchunguzi wa jinai dhidi ya waandamanaji waliofanya ghasia.

Hong Kong ambayo ni kitovu cha shughuhuli za kifedha na yenye mamlaka ya ndani, imekumbwa na  maandamano makubwa kwa wiki kadhaa sasa.

Waandamanaji hao wanapinga Muswada wa sheria ya kuwezesha raia wa Hong Kong kupelekwa China endapo watatakiwa kujibu mashtaka mahakamani.

Hapo juzi katika maadhimisho ya mwaka wa 22 tangu Uingereza kulirudisha jiji la Hong Kong katika mamlaka ya China, waandamani wenye misimamo mikali walivamia bunge na kuingia ndani kwa nguvu na  kutundika bendera ya enzi ya ukoloni wa Uingereza na kuchora huku kuandika vitu vya kuipinga China.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles