Na Mwandishi Wetu
Mahakama nchini Brazil imeamuru kuachiwa kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Michel Temer.
Mahakama hiyo imeeleza kwamba hapakuwepo na sababu yoyote ya kisheria ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa zamani.
Hakimu pia ameamuru kuachiwa kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati Moreira Franco. Temer na Franco walikamatwa kwa madai ya kuhusika na ufisadi katika shirika la serikali la mafuta Petrobras ambalo kwa miaka mingi limetikisa siasa za Brazil.