|Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesimamisha Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa Bank M na kuchukua usimamizi wa benki hiyo kukosa fedha za kujiendesha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Agosti 2, Gavana wa BoT, Profesa Florens Luoga amesema BoT imechukua hatua hiyo kulinda maslahi ya wateja wakopeshaji wote wanaohusika na shughulia ambazo azilikuwa zikiendeshwa na Benki M.
“Kwa mamlaka iliyopewa BoT chini ya sheria namba 56, (1) (g,) (3) cha sheria ya benki ya mwaka 2006, BoT imeamua kuchukua usimamizi wa Benki M kuanzia leo.
“Uamuzi huu umechululiwa baada ya kubainika benki hiyo ina upungufu mkubwa wa ukwasi kinyume na matakwa ya sheria ya kibenki na kanuni zake unaohatarisha usalama wa sekta za kifedha ambao kuendelea kutoa huduma kwa benki hiyo utahatarisha usalama wa amana za wateja wake.
“Kutokana na uamuzi huo, BoT imesimaisha bodi ya wakurugenzi na uongozi wa Banki M kuanzia leo, hivyo kutokana na uamuzi huo imemteua Meneja Msimamzi ambaye atakuwa na shughuli ya kusimamia benki hiyo kwa kipindi ambacho itakuwa chini usimamizi wa BoT,” amesema.
Pamoja na mambo mengine, Profesa Luoga amesema katika muda usiozidi siku 90 kuanzia sasa shuguli za utoaji wa huduma za kibenki katika benki hiyo, zitasimama kuipa nafasi BoT kutathimini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.