ROME, Italia
MKUU wa zamani wa kampuni ya kutengeneza magari ya Fiat Chrysler Automobiles (FCA), inayomilikiwa kwa ubia na Italia na Marekani, Sergio Marchionne amefariki dunia jana.
Marchionne, ambaye alijiuzulu Jumamosi kutokana na afya yake kudhoofika, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 66, FCA imesema.
FCA imetoa taarifa kwa Exor, familia iliyoanzisha kampuni ya Fiat na wanahisa wa FCA, ikimnukuu Mwenyekiti wake, John Elkann.
“Kwa bahati mbaya, kile tulichohofu kimetokea. Sergio Marchionne ameaga dunia,” Elkann alisema.
Mwingereza Mike Manley aliteuliwa wiki iliyopita kuwa Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa FCA baada ya Marchionne kujiuzulu Jumamosi iliyopita kufuatia hali yake kiafya kudhoofu.